Zab 18:25-29
Zab 18:25-29 SUV
Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu; Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi. Maana Wewe utawaokoa watu wanaoonewa, Na macho ya kiburi utayadhili. Kwa kuwa Wewe unaiwasha taa yangu; BWANA Mungu wangu aniangazia giza langu. Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.