Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 145:1-13

Zab 145:1-13 SUV

Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele. BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani. Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu. Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu. Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako. Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako. BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi. Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako. Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.

Soma Zab 145

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 145:1-13

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha