Zab 136:23-26
Zab 136:23-26 SUV
Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.