Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 119:81-88

Zab 119:81-88 SUV

Nafsi yangu imefifia kwa kuutamani wokovu wako, Nimelingojea neno lako. Macho yangu yamefifia kwa kuitazamia ahadi yako, Nisemapo, Lini utakaponifariji? Maana nimekuwa kama kiriba katika moshi, Sikuzisahau amri zako. Siku za mtumishi wako ni ngapi, Lini utakapowahukumu wale wanaonifuatia? Wenye kiburi wamenichimbia mashimo, Ambao hawaifuati sheria yako. Maagizo yako yote ni amini, Wananifuatia bure, unisaidie. Walikuwa karibu na kunikomesha katika nchi, Lakini sikuyaacha mausia yako. Unihuishe kwa fadhili zako, Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.

Soma Zab 119

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha