Zab 119:129-133
Zab 119:129-133 SUV
Shuhuda zako ni za ajabu, Ndiyo maana roho yangu imezishika. Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga. Nalifunua kinywa changu nikatweta, Maana naliyatamani maagizo yako. Unigeukie, unirehemu mimi, Kama iwahusuvyo walipendao jina lako. Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako, Uovu usije ukanimiliki.