Zab 119:12-16
Zab 119:12-16 SUV
Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako. Kwa midomo yangu nimezisimulia Hukumu zote za kinywa chako. Nimeifurahia njia ya shuhuda zako Kana kwamba ni mali mengi. Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako. Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.