Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 119:113-120

Zab 119:113-120 SUV

Watu wa kusita-sita nawachukia, Lakini sheria yako naipenda. Ndiwe sitara yangu na ngao yangu, Neno lako nimelingojea. Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, Niyashike maagizo ya Mungu wangu. Unitegemeze sawasawa na ahadi yako, nikaishi, Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu. Unisaidie nami nitakuwa salama, Nami nitaziangalia amri zako daima. Umewakataa wote wazikosao amri zako, Kwa maana hila zao ni uongo. Wabaya wa nchi pia umewaondoa kama takataka, Ndiyo maana nimezipenda shuhuda zako. Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako.

Soma Zab 119

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha