Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 115

115
Unyonge wa Sanamu na Ukuu wa Mungu
1 # Isa 48:11; Eze 36:32 Ee BWANA, kutukuza usitutukuze sisi,
Bali ulitukuze jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako,
Kwa ajili ya uaminifu wako.
2 # Zab 42:3,10; 79:10; Yoe 2:17 Kwa nini mataifa kusema,
Yuko wapi Mungu wao?
3 # 1 Nya 16:26; Zab 135:6; Dan 4:35 Lakini Mungu wetu yuko mbinguni,
Alitakalo lote amelitenda.
4 # Kum 4:28; Zab 135:15-18; Isa 40:19; Yer 20:3; Hos 8:6; 1 Kor 10:19,20; Ufu 9:20 Sanamu zao ni fedha na dhahabu,
Kazi ya mikono ya wanadamu.
5Zina vinywa lakini hazisemi,
Zina macho lakini hazioni,
6Zina masikio lakini hazisikii,
Zina pua lakini hazisikii harufu,
7Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi,
Wala hazitoi sauti kwa koo zake.
8 # Zab 135:18; Isa 44:9,10; Yon 2:8; Hab 2:18 Wazifanyao watafanana nazo,
Kila mmoja anayezitumainia.
9 # Zab 33:20; Mit 30:5 Enyi Israeli, mtumainini BWANA;
Yeye ni msaada wao na ngao yao.
10 # Mal 2:7 Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA;
Yeye ni msaada wao na ngao yao.
11Enyi mmchao BWANA, mtumainini BWANA;
Yeye ni msaada wao na ngao yao.
12 # Efe 1:3 BWANA ametukumbuka,
Naye atatubariki sisi.
Ataubariki mlango wa Israeli,
Ataubariki mlango wa Haruni,
13 # Law 26:3; Kum 11:27; Zab 24:4; Mit 10:6; Ufu 11:18; 19:5 Atawabariki wamchao BWANA,
Wadogo kwa wakubwa.
14BWANA na awaongeze ninyi,
Ninyi na watoto wenu.
15 # Mwa 14:19; 1:1; Zab 96:5 Na mbarikiwe ninyi na BWANA,
Aliyezifanya mbingu na nchi.
16Mbingu ni mbingu za BWANA,
Bali nchi amewapa wanadamu.
17Sio wafu wamsifuo BWANA,
Wala wo wote washukao kwenye kimya;
18 # Zab 145:2; Dan 2:20 Bali sisi tutamhimidi BWANA,
Tangu leo na hata milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 115: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha