Zab 11:4-7
Zab 11:4-7 SUV
BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawajaribu wanadamu. BWANA humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu. Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa hari, Na viwe fungu la kikombe chao. Kwa kuwa BWANA ndiye mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watamwona uso wake.