Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 102:1-13

Zab 102:1-13 SUV

Ee BWANA, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie. Usinifiche uso wako siku ya shida yangu, Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi. Maana siku zangu zinatoweka kama moshi, Na mifupa yangu inateketea kama kinga. Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu. Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwangu Mifupa yangu imegandamana na nyama yangu. Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani, Na kufanana na bundi wa mahameni. Nakesha, tena nimekuwa kama shomoro Aliye peke yake juu ya nyumba. Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu Huapa kwa kunitaja mimi. Maana nimekula majivu kama chakula, Na kukichanganya kinywaji changu na machozi. Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira yako; Maana umeniinua na kunitupilia mbali. Siku zangu zi kama kivuli kilichotandaa, Nami ninanyauka kama majani. Bali Wewe, BWANA utaketi ukimiliki milele, Na kumbukumbu lako kizazi hata kizazi. Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.

Soma Zab 102

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha