Mit 7:1-4
Mit 7:1-4 SUV
Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke.