Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 29:1-14

Mit 29:1-14 SUV

Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafula, wala hapati dawa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua. Apendaye hekima humfurahisha babaye; Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali. Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua. Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake. Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi. Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini; Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue. Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu. Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha. Wamwagao damu humchukia mtu mkamilifu; Bali wenye haki humtunza nafsi yake. Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza. Mwenye kutawala akisikiliza uongo; Basi watumishi wake wote watakuwa waovu. Maskini na mdhalimu hukutana pamoja; BWANA huwatia nuru macho yao wote wawili. Mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; Kiti chake cha enzi kitathibitika milele.

Soma Mit 29