Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 23:9-18

Mit 23:9-18 SUV

Usiseme masikioni mwa mpumbavu; Maana atadharau hekima ya maneno yako. Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima; Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako. Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa. Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu. Mwanangu, kama moyo wako una hekima, Moyo wangu utafurahi, naam, moyo wangu; Naam, viuno vyangu vitafurahi, Midomo yako inenapo maneno mema. Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa; Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika.

Soma Mit 23

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mit 23:9-18

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha