Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 23:26-35

Mit 23:26-35 SUV

Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba. Naam, huotea kama mnyang’anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu. Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.

Soma Mit 23

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mit 23:26-35

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha