Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 14:1-12

Mit 14:1-12 SUV

Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha BWANA; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau. Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi. Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe; Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi. Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo. Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate; Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu. Toka mbele ya uso wa mpumbavu, Maana hutaona kwake midomo ya maarifa. Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki. Moyo huujua uchungu wa nafsi yake, Wala mgeni haishiriki furaha yake. Nyumba ya mtu mbaya itabomolewa; Bali hema ya mwenye haki itafanikiwa. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Soma Mit 14