Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Flp 4

4
1 # 2 Kor 1:14; 1 The 2:19,20 Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.
Himizo
2Namsihi Euodia, namsihi na Sintike, wawe na nia moja katika Bwana. 3#Zab 69:28; Lk 10:20Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
4 # Flp 3:1; 2 Kor 13:11 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. 5#Ebr 10:37; Yak 5:8,9Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. 6#Mt 6:25-34; Kol 4:2; 1 Pet 5:7; Zab 145:18; Yn 14:27Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7#Kol 3:15Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
8 # Rum 12:17 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. 9#1 The 5:23; Rum 16:20; 1 Kor 14:33Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
Shukrani kwa Zawadi za Wafilipi
10Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi. 11#1 Tim 6:6Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. 12#2 Kor 6:10Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. 13#2 Kor 12:10; 2 Tim 4:17Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. 14Lakini mlifanya vema, mliposhiriki nami katika dhiki yangu. 15#2 Kor 11:9Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. 16#Mdo 17:1Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja. 17#1 Kor 9:11Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu. 18#Kut 29:18; Eze 20:41; Flp 2:25Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu. 19Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. 20Sasa atukuzwe Mungu, Baba yetu, milele na milele. Amina.
Salamu na Baraka
21Mnisalimie kila mtakatifu katika Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami wawasalimu. 22#Flp 1:13Watakatifu wote wawasalimu, hasa wao walio wa nyumbani mwa Kaisari.
23Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.

Iliyochaguliwa sasa

Flp 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha