Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Neh 7:70-72

Neh 7:70-72 SUV

Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni za dhahabu elfu moja, na mabakuli hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini. Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu ishirini elfu, na mane za fedha elfu mbili na mia mbili. Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu ishirini elfu, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.

Soma Neh 7