Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nah UTANGULIZI

UTANGULIZI
Nahumu mkazi wa mji wa Elkoshi, alitoa ujumbe wa hukumu kwa mji wa Ninawi, makao makuu ya Ashuru. Kama maana ya jina, yaani “faraja” au “mfariji” lilivyo ndivyo amekuwa mtoa ujumbe wa faraja nyingi kwa watu wa Yuda.
Karne ya nane Kabla ya Kristo Kuzaliwa taifa la Ashuru lilipata nguvu nyingi, lilipanua himaya yake kwa kuteka mataifa madogo ya Palestina. Yuda walitozwa ushuru na kodi kubwa. Baada ya miaka kama mia moja Ashuru lilipungua nguvu, Babeli iliinuka kijeshi na kimamlaka. Adui wa Ashuru walifurahi. Yuda alitegemea hukumu ya Mungu kutolewa kwa taifa jeuri na katili (3:19).
Ujumbe wa Nahumu umewekwa kwa njia ya mashairi kwamba Mungu wa haki ataadhibu wenye ukatili na udhalimu na wote wapingao matakwa yake (1:11-15; 2:1). Wenye maisha yasiyo adili nao wataadhibiwa. Ninawi utaadhibiwa kwa kuwa umedhulumu Yuda (1:12-13) na mataifa mengine (3:1-7). Yuda itaokolewa (1:2). Unabii wa Nahumu ulitimia mwaka 612 Kabla ya Kristo Kuzaliwa, Ninawi ulipotekwa na Wababeli.
Yaliyomo:
1. Mamlaka ya Mungu, Sura 1
2. Maangamizi kwa Ninawi, Sura 2
3. Dhambi ya Ninawi, Sura 3

Iliyochaguliwa sasa

Nah UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha