Mk 13:5-8
Mk 13:5-8 SUV
Yesu akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye. Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, nao watadanganya wengi. Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali; kutakuwako na njaa; hayo ndiyo mwanzo wa utungu.