Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mk 13:14-19

Mk 13:14-19 SUV

Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo! Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi. Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe.

Soma Mk 13