Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mt 22

22
Mfano wa Karamu ya Arusi
1Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema, 2#Lk 14:16-24#Yn 3:29Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. 3Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja. 4#Mt 21:36Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini. 5Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake; 6nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua. 7#Mt 24:2Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. 8Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. 9#Mt 13:47; 21:43Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini. 10Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni. 11Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi. 12Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. 13#Mt 8:12; 25:30; Lk 13:28Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. 14Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.
Swali juu ya Kulipa Kodi
15 # Mk 12:13-17; Lk 20:20-26 # Yn 8:6 Ndipo Mafarisayo wakaenda zao, wakafanya shauri, jinsi ya kumtega kwa maneno. 16#Mk 3:6; Yn 3:2Wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu. 17Basi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo? 18Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki? 19Nionyesheni fedha ya kodi. Nao wakamletea dinari. 20Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii, na anwani hii? 21#Rum 13:7Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu. 22#Yn 8:9Waliposikia, walistaajabu, wakamwacha, wakaenda zao.
Swali Kuhusu Ufufuo
23 # Mk 12:18-27; Lk 20:27-40 # Mdo 23:8 Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, 24#Kum 25:5,6; Mwa 38:8wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. 25Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. 26Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. 27Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. 28Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye. 29Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu. 30Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni. 31Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, akisema, 32#Kut 3:6; Mt 8:11Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. 33Na makutano waliposikia, walishangaa kwa mafunzo yake.
Amri iliyo Kuu Zaidi
34 # Mk 12:28-31; Lk 10:25-28 Na Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja. 35#Lk 10:25-28Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; 36Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37#Kum 6:5Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39#Law 19:18Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40#Mt 7:12; Rum 13:10; Gal 5:14Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Swali kuhusu Mwana wa Daudi
41 # Mk 12:35-37; Lk 20:41-44 Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo? 42#Yn 7:42Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi. 43Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,
44 # Zab 110:1; Mt 26:64 Bwana alimwambia Bwana wangu,
Uketi mkono wangu wa kuume,
Hata niwawekapo adui zako
Kuwa chini ya miguu yako?
45Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe? 46Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.

Iliyochaguliwa sasa

Mt 22: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha