Lk 22:1-3
Lk 22:1-3 SUV
Ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Sikukuu ya Pasaka. Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu. Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara.