Law 22:31-33
Law 22:31-33 SUV
Kwa hiyo mtayashika maagizo yangu, na kuyafanya; mimi ndimi BWANA. Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi, niliyewaleta mtoke nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA.


