Walawi 22:31-33 - Compare All Versions
Walawi 22:31-33 BHN (Biblia Habari Njema)
“Kwa hiyo mtazishika na kuzitekeleza amri zangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu. Msilikufuru jina langu takatifu, kwani ni lazima niheshimiwe miongoni mwa watu wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu ndiye ninayewaweka wakfu. Mimi ndimi niliyewatoa nchini Misri ili niwe Mungu wenu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”
Walawi 22:31-33 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo mtayashika maagizo yangu, na kuyafanya; mimi ndimi BWANA. Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi, niliyewaleta mtoke nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA.
Walawi 22:31-33 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo mtayashika maagizo yangu, na kuyafanya; mimi ndimi BWANA. Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi, niliyewaleta mtoke nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA.
Walawi 22:31-33 NEN (Neno)
“Shikeni maagizo yangu na kuyafuata. Mimi ndimi BWANA. Msilinajisi Jina langu takatifu. Lazima nikubalike kuwa mtakatifu kwa Waisraeli. Mimi ndimi BWANA ninayewafanya watakatifu, na niliyewatoa katika nchi ya Misri niwe Mungu wenu. Mimi ndimi BWANA.”