Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 42:1-5

Ayu 42:1-5 SUV

Ndipo Ayubu akamjibu BWANA, na kusema. Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie. Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona.

Soma Ayu 42