Ayu 38:8-11
Ayu 38:8-11 SUV
Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni. Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia, Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango, Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?