Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 36

36
Elihu Asifia Wema wa Mungu
1Tena Elihu akaendelea na kusema,
2Ningojee kidogo nami nitakueleza;
Kwa kuwa nikali na maneno kwa ajili ya Mungu.
3Nitayaleta maarifa yangu kutoka mbali,
Nami nitampa haki Muumba wangu.
4Kwani yakini maneno yangu si ya uongo;
Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe.
5Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote;
Ana uweza katika nguvu za fahamu.
6Hauhifadhi uhai wa waovu;
Lakini huwapa wateswao haki yao.
7 # Zab 113:8 Yeye hawaondolei macho yake wenye haki;
Lakini pamoja na wafalme huwaweka
Katika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.
8 # Zab 107:10 Nao wakifungwa kwa pingu,
Wakitwaliwa kwa kamba za mateso;
9Ndipo huwaonyesha matendo yao,
Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna.
10Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo,
Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu.
11 # Ayu 11:13-19; Isa 1:19; 1 Tim 4:8; Yak 5:5 Kama wakisikia na kumtumikia,
Watapisha siku zao katika kufanikiwa,
Na miaka yao katika furaha.
12Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga,
Nao watakufa pasipo maarifa.
13Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasira
Hawalilii msaada hapo awafungapo.
14Wao hufa wakali vijana,
Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu.
15Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake,
Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu.
16Naam, yeye angekuongoza utoke katika msiba
Hata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge;
Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta.
17Lakini umejaa hukumu ya waovu;
Hukumu na haki hukushika.
18Basi ujitunze, isije hasira ikakuvuta hata ukafanya mzaha;
Wala usikubali ukuu wa ukombozi ukugeuze.
19Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu,
Au uwezo wote wa nguvu zako?
20Usiutamani usiku,
Wakati watu wakatwapo katika mahali pao.
21 # Ebr 11:25 Jitunze, usiutazame uovu;
Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu.
22 # Isa 40:13; Rum 11:34; 1 Kor 2:16 Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake;
Ni nani afundishaye kama yeye?
23 # Kum 32:4 Ni nani aliyemwagiza njia yake?
Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki?
Elihu Atangaza Ukuu wa Mungu
24 # Zab 33:4; Dan 4:37; Yer 9:24; 1 Kor 1:31; 2 Kor 10:17; Ufu 15:3 Kumbuka kuitukuza kazi yake,
Watu waliyoiimbia.
25 # Rum 1:19 Wanadamu wote wameitazama;
Watu huiangalia kwa mbali
26 # 1 Kor 13:12; Zab 90:2; Ebr 1:12 Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui;
Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27Kwani yeye huvuta juu matone ya maji,
Yamwagikayo katika mvua kutoka kungeni mwake;
28Ambayo mawingu yainyesha
Na kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi.
29Naam, mtu aweza kuelewa na matandazo ya mawingu,
Ngurumo za makao yake?
30Tazama, yeye huutandaza mwanga wake, umzunguke;
Naye hufunika vilindi vya bahari.
31Kwani huwahukumu kabila za watu kwa njia hizi;
Hutoa chakula kwa ukarimu.
32Yeye huifunika mikono yake kwa umeme;
Na kuuagiza shabaha utakayopiga.
33Mshindo wake hutoa habari zake,
Anayewaka hasira juu ya uovu.

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 36: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha