Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yer 19

19
Kuvunjika kwa Gudulia
1 # Eze 8:11 BWANA akasema hivi, Enenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani; 2#Yos 15:8; 2 Nya 28:3; Mit 1:20; 2 Fal 23:10; Yer 7:30-32; 32:34-35ukatoke uende mpaka bonde la mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia, 3ukisema, Lisikieni neno la BWANA, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka. 4#Kum 28:20; Isa 65:11; Yer 17:13; 2 Fal 21:16Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia; 5#Law 18:21nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu; 6#Yos 15:8basi, angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo. 7#Law 26:17; Kum 28:25,26; Yer 9:21; 7:33; Zab 79:2; Ufu 19:18Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao. 8#Law 26:22; 1 Fal 9:8; Yer 18:16; Omb 2:15,16; Sef 2:15Nami nitaufanya mji huu kuwa kitu cha kushangaza watu, na kuzomewa; kila mtu apitaye karibu nao atashangaa, na kuzomea kwa sababu ya mapigo yake. 9#Law 26:29; Kum 28:53; Isa 9:20; Omb 4:10Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawadhiikisha. 10#Yer 51:63Ndipo hapo utalivunja gudulia lile, mbele ya macho ya watu wale waendao pamoja nawe, 11#Zab 2:9; Isa 30:14; Omb 4:2; Yer 7:32na kuwaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika. 12Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa, asema BWANA, nao wakaao humo, hata kufanya mji huu kuwa kama Tofethi; 13#2 Fal 23:10; Sef 1:5; Yer 32:29; 7:18na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa.
14 # 2 Nya 20:5 Kisha Yeremia akatoka huko Tofethi, huko ambako BWANA alimtuma atoe unabii; naye akasimama katika ua wa nyumba ya BWANA, akawaambia watu wote, 15#2 Nya 36:16,17; Yer 7:26; Zek 7:11-14; Mdo 7:51,52BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaleta juu ya mji huu, na juu ya vijiji vyake vyote, mabaya yote niliyoyanena juu yake; kwa sababu wamefanya shingo zao kuwa ngumu, kusudi wasiyasikie maneno yangu.

Iliyochaguliwa sasa

Yer 19: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha