Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yer 17

17
Dhambi ya Yuda na Adhabu
1 # Ayu 19:24; Mit 3:3; 2 Kor 3:3 Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu; 2#2 Fal 16:4; 2 Nya 24:18; Isa 1:29na wakati huo watoto wao wazikumbuka madhabahu zao, na maashera yao, karibu na miti yenye majani mabichi juu ya milima mirefu. 3#Yer 15:13Ee mlima wangu wa uwandani, nitatoa mali zako na hazina zako zote ziwe nyara, na mahali pako palipoinuka, kwa sababu ya dhambi, katika mipaka yako yote. 4#Yer 16:13Nawe, naam, wewe nafsi yako, utaachana na urithi wako niliokupa; nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana umewasha moto katika hasira yangu, utakaowaka milele.
5 # Isa 30:1 BWANA asema hivi,
Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu,
Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake
Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
6 # Ayu 20:17 Maana atakuwa kama fukara nyikani,
Hataona yatakapotokea mema;
Bali atakaa jangwani palipo ukame,
Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7 # Zab 2:12; Mit 16:20 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA,
Ambaye BWANA ni tumaini lake.
8 # Zab 1:3 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji,
Uenezao mizizi yake karibu na mto;
Hautaona hofu wakati wa hari ujapo,
Bali jani lake litakuwa bichi;
Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua,
Wala hautaacha kuzaa matunda.
9 # Mwa 6:5 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? 10#1 Sam 16:7; 1 Nya 28:9; Zab 7:9; 139:23; 62:12; Yer 11:20; 20:12; 32:19; Mit 17:3; Rum 8:27; 2:6; Ufu 2:23Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake. 11#Lk 12:20Kama kware akusanyaye makinda asiyoyazaa, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya siku zake zitaachana naye, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.
12Kiti cha enzi, cha utukufu, kilichowekwa juu tangu mwanzo, ndicho mahali patakatifu petu. 13#Zab 73:27; Yer 2:26; Isa 1:28; 65:13; Eze 16:63; 36:32; Dan 12:2; Lk 10:20Ee BWANA, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. Wao watakaojitenga nami wataandikwa katika mchanga, kwa sababu wamemwacha BWANA, kisima cha maji yaliyo hai.
Yeremia Aomba Kuthibitishiwa
14Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu. 15#Isa 5:19; Eze 12:22; Amo 5:18; 2 Pet 3:4Tazama, wao waniambia, Neno la BWANA liko wapi? Na lije, basi. 16Mimi hapa sikufanya haraka kuacha kuwa mchungaji nyuma yako; wala sikuitamani siku ya maradhi ya kufisha; wewe unajua; yaliyotoka midomoni mwangu yalikuwa mbele za uso wako. 17Usiwe sababu ya hofu kuu kwangu mimi; wewe ndiwe uliye kimbilio langu siku ya uovu. 18Na waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi; na waone hofu kuu, lakini mimi nisione hofu kuu; ulete juu yao siku ya uovu; uwaangamize maangamizo maradufu.
Tukuza Siku ya Sabato
19BWANA akaniambia hivi, Enenda ukasimame katika lango la wana wa watu hawa, waingiapo wafalme wa Yuda, na watokeapo, na katika malango yote ya Yerusalemu, 20#Zab 49:1; Yer 19:3; 22:2; Eze 2:7; 3:17; Hos 5:1; Mik 3:1ukawaambie, Lisikieni neno la BWANA, enyi wafalme wa Yuda, na Yuda wote, nanyi wenyeji wote wa Yerusalemu, ninyi mwingiao kwa malango haya; 21#Hes 15:32; Neh 13:15-22BWANA asema hivi, Jihadharini nafsi zenu, msichukue mzigo wo wote siku ya sabato, wala msiulete ndani kwa malango ya Yerusalemu; 22#Kut 20:8-10; 23:12; 31:13; Eze 20:12; Kum 5:12-14wala msitoe mzigo katika nyumba zenu siku ya sabato, wala msifanye kazi yo yote; bali itakaseni siku ya sabato, kama nilivyowaamuru baba zenu; 23lakini hawakusikiliza, wala hawakutega masikio yao, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, ili wasisikilize wala wasipokee mafundisho. 24Na itakuwa, kama mkinisikiliza mimi kwa bidii, asema BWANA, msiingize mzigo wo wote kwa malango ya mji huu siku ya sabato, bali mkiitakasa siku ya sabato, bila kufanya kazi yo yote siku hiyo; 25#Kum 4:40ndipo watakapoingia wafalme na wakuu kwa malango ya mji huu; wataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kupanda magari na farasi, wao, na wakuu wao, watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; na mji huu utakaa hata milele. 26#Zek 7:7; Zab 107:22Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela,#17:26 Shefela tafsiri yake ni Nchi ya mabonde. na milima, na upande wa Negebu,#17:26Negebu tafsiri yake ni Nchi ya kusini. wakileta sadaka za kuteketezwa, na dhabihu, na sadaka za unga, na ubani, wakileta pia sadaka za shukrani, nyumbani kwa BWANA 27#Omb 4:11; Amo 1:4; 2 Fal 25:9Lakini kama hamtaki kunisikiliza, kuitakasa siku ya sabato, kutokuchukua mzigo na kuingia kwa malango ya Yerusalemu siku ya sabato; basi, nitawasha moto malangoni mwake, nao utaziteketeza nyumba za enzi za Yerusalemu, wala hautazimika.

Iliyochaguliwa sasa

Yer 17: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha