Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 44

44
Baraka za Mungu kwa Israeli
1 # Isa 41:8; Yer 30:10 Lakini sikia sasa, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na Israeli, niliyekuchagua; 2#Kum 32:15BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua. 3#Mal 3:10; Yn 7:38Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa; 4nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji. 5#Kut 13:9; Neh 9:38Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.
6 # Isa 48:12; 43:1; 41:4; Ufu 1:8,17; 2:8; 22:13 BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. 7Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze. 8#Kum 4:35; 1 Sam 2:2; 2 Sam 22:32Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.
Upumbavu wa Kuabudu Sanamu
9 # Isa 41:24; 42:17-20; Kum 4:28; Zab 115:4 Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike. 10#Yer 10:5; Hab 2:18Ni nani aliyejichongea mungu mmoja, au aliyesubu sanamu isiyofaa kitu? 11#Zab 97:7; Isa 42:17Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja. 12#Isa 40:19Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kazi kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia. 13Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwa mfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani. 14Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha. 15Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia. 16Sehemu moja huiteketeza; kwa sehemu nyingine hula nyama; huoka chakula kiokwacho, akashiba; naam, huota moto, akasema, Aha, nimeota moto, nimeona moto; 17na kwa sehemu iliyobakia hufanya mungu, yaani, sanamu yake ya kuchonga; husujudu mbele yake akaiabudu, akaiomba, akasema, Uniokoe; maana wewe u mungu wangu. 18#Zab 81:12; Isa 45:20; Rum 11:8-10; 2 The 2:11Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu. 19Wala hapana atiaye moyoni, wala hapana maarifa, wala fahamu kusema, Nimeteketeza sehemu motoni, naam, pia nimeoka mkate juu ya makaa yake; nimeoka nyama nikaila; nami, je! Kilichobaki nikifanye kuwa chukizo? Je! Nisujudie shina la mti? 20#Hos 4:12; Rum 1:21; 2 The 2:11Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?
Israeli Haujasahauliwa
21Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi. 22#Isa 1:18; 43:25; 53:11,12; Yer 33:8; Mik 7:18,19; Kol 1:14; Isa 43:1; 1 Kor 6:20; 1 Pet 1:18,19Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.
23 # Zab 69:34; Isa 42:10; Ufu 18:20 Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo;
Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi;
Pazeni nyimbo, enyi milima;
Nawe, msitu, na kila mti ndani yake.
Maana BWANA amemkomboa Yakobo,
Naye atajitukuza katika Israeli.
24 # Ayu 19:25; 9:8; Isa 43:1,14; 40:22; Zab 104:2 BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami? 25#Yer 50:36; 1 Kor 1:20Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga; 26#Zek 1:6; Mt 5:18nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka; 27#Yer 50:38niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako; 28#2 Nya 36:22,23; Ezr 1:2nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 44: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha