Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 43

43
Ahadi ya Matengenezo na Ulinzi
1 # Isa 44:6; 42:6; 1 Kor 1:9; 2 Tim 1:9 Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. 2#Zab 66:12; Kum 31:6-8; Dan 3:25Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. 3#Mit 21:18Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. 4#Kut 19:5,6Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. 5#Isa 41:10,14; 44:2Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi; 6nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia. 7#Isa 63:19; 29:23; Zab 100:3; Yn 3:3; 2 Kor 5:17; Efe 2:10Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya. 8#Isa 6:9; 42:19Walete vipofu walio na macho, na viziwi walio na masikio. 9Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonyesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli. 10#Yn 1:7; Mdo 1:8; Ebr 12:1; Ufu 1:5; Isa 44:8; 41:8Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. 11Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi. 12#Kum 32:16Nimetangaza habari, nimeokoa, nimeonyesha, na hapakuwa mungu wa kigeni kati yenu; kwa sababu hiyo ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, nami ni Mungu. 13#Zab 90:2; Mit 8:23; Mik 5:2; Mt 19:26Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
14BWANA, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Kwa ajili yenu nimetuma ujumbe Babeli nami nitawashusha wote mfano wa wakimbizi, naam, Wakaldayo, katika merikebu zao walizozifurahia. 15#Hos 13:10Mimi ni BWANA, Mtakatifu wenu, Muumba wa Israeli, mfalme wenu. 16#Zab 77:19BWANA asema hivi, yeye afanyaye njia katika bahari; na mahali pa kupita katika maji yenye nguvu; 17#Kut 14:4atoaye gari na farasi, jeshi la askari na uwezo; wamelala, hawataondoka; wametoweka, wamezimwa mfano wa utambi. 18Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. 19#2 Kor 5:17; Ufu 21:5Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. 20#Isa 48:21; Lk 1:74; Efe 1:5Wanyama wa kondeni wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu; 21watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu. 22#Mal 1:13Lakini hukuniita, Ee Yakobo, bali umechoka nami, Ee Israeli. 23Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani. 24#Isa 1:14; Mal 2:17; Yud 1:4Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako. 25#Isa 44:22; Yer 31:34; Mik 7:18,19; Eze 36:22Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. 26Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. 27#Rum 5:12Baba yako wa kwanza alifanya dhambi, na wakalimani wako wameniasi. 28#Isa 47:6; Omb 2:2; Zab 79:4; Yer 24:9; Dan 9:11; Zek 8:13Kwa hiyo nitawatia unajisi wakuu wa patakatifu, nami nitamfanya Yakobo kuwalaani, na Israeli kuwa tukano.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 43: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha