Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 39

39
Wajumbe kutoka Babeli Wakaribishwa
1 # 2 Fal 20:12 Wakati huo Merodaki-baladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana amepata habari kwamba amekuwa hawezi, na kwamba amepona. 2#2 Nya 32:31Hezekia akawafurahia, akawaonyesha nyumba yake yenye vitu vyake vya thamani, fedha na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yote yenye silaha zake za vita, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake; hapakuwa na kitu nyumbani mwake wala katika ufalme wake asichowaonyesha. 3Ndipo Isaya nabii akamwendea mfalme Hezekia, akamwambia, Watu hawa walisema nini? Nao wametoka wapi kuja kwako? Hezekia akasema, Wametoka katika nchi iliyo mbali, wakaja kwangu toka Babeli. 4Ndipo akasema, Wameona nini katika nyumba yako? Hezekia akajibu, Wameviona vitu vyote vilivyomo nyumbani mwangu; hapana kitu katika hazina zangu nisichowaonyesha. 5Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, Basi, lisikie neno la BWANA wa majeshi. 6#Law 26:33; Kum 28:64; 1 Fal 14:15; 2 Nya 36:18; Amo 5:27Tazama, siku zinakuja, ambazo vitu vyote vilivyomo nyumbani mwako, na hivyo vilivyowekwa akiba na baba zako hata leo, vitachukuliwa mpaka Babeli; hapana kitu cho chote kitakachosalia; asema BWANA. 7#Dan 1:1-7; 2 Fal 24:10-16; 2 Nya 36:10Na baadhi ya wana wako utakaowazaa, watakaotoka kwako, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli. 8#1 Sam 3:18Ndipo Hezekia akamwambia Isaya, Neno la BWANA ulilolinena ni jema. Tena akamwambia, Maana itakuwapo amani na kweli katika siku zangu mimi.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 39: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha