Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 22

22
Onyo la Kuharibiwa kwa Yerusalemu
1Ufunuo juu ya bonde la maono.
Sasa una nini, wewe,
Hata umepanda pia juu ya dari za nyumba?
2Ewe uliyejaa makelele,
Mji wa ghasia, mji wenye furaha;
Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga,
Wala hawakufa vitani.
3Wakuu wako wote wamekimbia pamoja,
Wamefungwa wasiutumie upinde.
Wote walioonekana wamefungwa pamoja,
Wamekimbia mbali sana.
4Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu. 5#Est 3:15; Omb 1:5Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima. 6#Isa 21:2; Yer 49:35Na Elamu wameshika podo, pamoja na magari ya vita, na watu wenye kupanda farasi; na Kiri wameifunua ngao. 7Hata ikawa mabonde yako mateule yamejaa magari ya vita, nao wapandao farasi wamejipanga wakielekea malango. 8#1 Fal 7:2Kisha alikiondoa kifuniko cha Yuda, nawe siku hiyo ulivitazama vyombo vya vita katika nyumba ya mwituni. 9#2 Fal 20:20; 2 Nya 32:4; Wim 4:4Nanyi mlipaona mahali palipobomoka katika mji wa Daudi ya kuwa ni pengi, nanyi mliyakusanya maji ya birika la chini. 10Nanyi mlizihesabu nyumba za Yerusalemu, mkazibomoa nyumba ili kuutia nguvu ukuta. 11#Neh 3:16Nanyi mlifanya birika la maji katikati ya kuta mbili, la kuwekea maji ya birika la kale; lakini hamkumwangalia yeye aliyeyafanya hayo, wala kumjali yeye aliyeyatengeneza zamani. 12Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung’oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia; 13#Isa 5:12; Amo 6:3; Lk 17:26-29; Isa 56:12; 1 Kor 15:32na kumbe! Furaha, na kuchekelea, na kuchinja ng’ombe, na kuchinja kondoo, na kula nyama, na kunywa mvinyo; tule, tunywe, kwa maana kesho tutakufa. 14#1 Sam 3:14; Eze 24:13Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Shutuma kwa Maofisa wa Kujipendekeza
15 # 2 Fal 18:37; Isa 36:3; 1 Fal 4:6 Bwana, BWANA wa majeshi, asema hivi, Haya! Enenda kwa huyu mtunza hazina, yaani, Shebna, aliye juu ya nyumba, ukamwambie, 16Unafanyaje hapa? Nawe una nani hapa? Hata ukachimba kaburi hapa; ukamchimbia kaburi huko juu, na kumchongea makao katika jabali! 17Tazama, BWANA atakutupa kwa nguvu, kama mtu mwenye nguvu; naam, atakuzonga-zonga. 18Hakika atakukunja na kukutupa kama mpira, mpaka nchi iliyo mbali; huko utakufa, na magari ya utukufu wako yatakuwa kuko huko, ewe uliye aibu ya nyumba ya bwana wako. 19Nami nitakusukuma na kukutoa katika mahali pako, naye atakushusha utoke hapa usimamapo. 20#2 Fal 18:18Na itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia; 21#Ayu 29:16nami nitamvika vazi lako, nitamtia nguvu kwa mshipi wako, nami nitamkabidhi yeye mamlaka yako; naye atakuwa baba kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa nyumba ya Yuda. 22#Ufu 3:7Na ufunguo wa nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua. 23#Ezr 9:8Nami nitamkaza kama msumari mahali palipo imara; naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake. 24Nao wataangika juu yake utukufu wote wa nyumba ya baba yake; wazao wake na watoto wao, kila chombo kidogo tangu vyombo vya vikombe hata vyombo vya makopo vyote pia. 25Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, ule msumari uliokazwa katika mahali palipo imara utalegea; nao utakatwa na kuanguka chini, na ule mzigo uliokuwa juu yake utakatiliwa mbali; maana BWANA amesema haya.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 22: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha