Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ebr 5

5
1Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi; 2#Ebr 4:15awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu; 3#Law 9:7; 16:6na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi. 4#Kut 28:1Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. 5#Zab 2:7; Mdo 13:33Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia,
Ndiwe mwanangu,
Mimi leo nimekuzaa.
6 # Zab 110:4; Ebr 7:1 kama asemavyo mahali pengine,
Ndiwe kuhani milele
Kwa mfano wa Melkizedeki.
7 # Mt 26:36-46; Mk 14:32-42; Lk 22:39-46 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; 8#Flp 2:8na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; 9#Isa 45:17; Yn 17:1,5naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii; 10kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
Maonyo dhidi ya Uasi
11Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. 12#1 Kor 3:2; 1 Pet 2:2Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 13#Efe 4:14Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14#Flp 1:10; Rum 16:19; Mwa 2:17Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.

Iliyochaguliwa sasa

Ebr 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha