Hab 3:17-19
Hab 3:17-19 SUV
Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe; Walakini nitamfurahia BWANA Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.