Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 28

28
1 # Mwa 27:33 Basi Isaka akamwita Yakobo, akambariki, akamwagiza akamwambia, Usitwae mke wa binti za Kanaani. 2Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako. 3#Mwa 17:1,6Na Mungu Mwenyezi, akubariki, akuzidishe, na kukuongeza, ili uwe mkutano wa makabila. 4#Mwa 17:4-8; Mwa 12:2; 22:17; 1 Nya 29:15; Zab 39:12; 2 Kor 5:6,7; Ebr 11:9,13; 1 Pet 1:17; 2:11Akupe mbaraka wa Ibrahimu, wewe na uzao wako pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, Mungu aliyompa Ibrahimu. 5Basi Isaka akampeleka Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.
Esau Amwoa Binti wa Ishmaeli
6Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usitwae mke wa binti za Kanaani, 7na ya kuwa Yakobo amewatii babaye na mamaye, akaenda Padan-aramu. 8#Mwa 24:3Esau akaona ya kuwa binti za Kanaani hawakumpendeza Isaka, baba yake. 9#Mwa 25:13; 36:3Basi Esau akaenda kwa Ishmaeli akamtwaa Mahalathi, binti Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, ndugu wa Nebayothi, kuwa mkewe pamoja na wakeze aliokuwa nao.
Ndoto ya Yakobo katika Betheli
10 # Mdo 7:2 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. 11Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. 12#Yn 1:51; Mwa 41:1; Ayu 33:15; Ebr 1:14Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. 13#Mwa 13:14-15; Mwa 35:1; 48:3; 26:24Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. 14#Mwa 12:3; 22:18; Mwa 13:14-16; Kum 12:20Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. 15#Mwa 26:24; 35:6; 48:16; Zab 121:5; Kum 31:6; Hes 23:19Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
16 # Kut 3:5; Yos 5:15 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. 17Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. 18Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. 19#Amu 1:23; Hos 4:15Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. 20#Mwa 28:15; 31:13; Amu 11:30; 2 Sam 15:8; 1 Tim 6:8Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 21#Amu 11:31; 2 Sam 15:8; 19:24; Kum 26:17; 2 Fal 5:17nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu. 22#Mwa 35:7; Law 27:30Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

Iliyochaguliwa sasa

Mwa 28: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha