Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Eze 42:15-20

Eze 42:15-20 SUV

Basi, alipokuwa amekwisha kuipima nyumba ya ndani, akanileta nje, kwa njia ya lango lililokabili upande wa mashariki, akalipima pande zote. Akaupima upande wa mashariki kwa mwanzi wa kupimia, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote. Akaupima upande wa kaskazini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote. Akaupima upande wa kusini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia. Akageuka aelekee upande wa magharibi, akapima mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia. Alipima pande zake zote nne; lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali palipo pa watu wote.

Soma Eze 42

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Eze 42:15-20

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha