Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu cha Kutoka ni cha pili katika orodha ya vitabu vya Biblia. Jina la kitabu linatokana na masimulizi yanayohusu tukio maalumu la Waisraeli kuwekwa huru toka utumwani walikoishi kwa muda wa karne nne.
Kutoka kinasimulia utendaji wa Mungu katika kuondoka kwa Waisraeli Misri na kufanywa Agano Mlimani Sinai. Mungu alimchagua Musa akamfanya kuwa chombo chake. Musa ana uhusiano wa ana kwa ana na Mungu kuliko viongozi wote wa Waisraeli. Sadaka ya mwanakondoo wa Pasaka ni tendo la Mungu kuhukumu Wamisri na kukomboa Waisraeli. Agano linatoa mwongozo wenye kanuni na sheria za maisha kidini, kijamii na kitaifa.
Waisraeli kama taifa la Mungu wanajifunza na kuanza kumwelewa Mungu wao kawamba aliwachagua, ni mkombozi na mwokozi wao aida wakati wote ni mwaminifu. Ijapokuwa mara kadaa Waisraeli walinung’unika hata kuvunja Agano, Mungu aliendelea kuwaongoza, aliwakinga na maangamizi na kuwahifadhi. Ujumbe mkuu hapa ni kuwa uaminifu na utiifu ni muhimu sana.
Yaliyomo
1. Waisraeli utumwani Misri, Sura 1–12
(a) Waisraeli wateswa (1)
(b) Kuzaliwa, kuitwa, na kutumwa kwa Musa (2:1–7:13)
(c) Mapigo na Pasaka (7:14–12:36)
2. Waisraeli watoka Misri na kusafiri hadi Sinai, Sura 12:36–18:27
3. Agano la Sinai, Sura 18–24
4. Hema takatifu na mwongozo katika kuabudu, Sura 25–40

Iliyochaguliwa sasa

Kut UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha