Kut 21:12-16
Kut 21:12-16 SUV
Mtu awaye yote ampigaye mtu, hata akafa, hana budi atauawa huyo. Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonyesha mahali atakapopakimbilia. Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe. Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa. Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyo