Kut 13:3-5
Kut 13:3-5 SUV
Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa. Ninyi mwatoka leo katika mwezi wa Abibu. Itakuwa hapo BWANA atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi huu.