Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kum UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kumbukumbu la Torati ni kitabu cha tano katika mfuatano wa vitabu vya Biblia. Torati ni neno lenye asili ya Kiebrania kwa maana ya sheria au mwongozo. Hivyo jina la kitabu hiki linamaanisha “sheria iliyodurusiwa tena”, “nakala ya sheria” au “sheria iliyorudiwa” kabla ya Waisraeli kuingia katika Nchi ya Ahadi. Katika kitabu hiki Musa anawakumbusha Waisraeli, wengi wao wakiwa kizazi kipya, yale yote Mungu aliyowaambia na aliyowatendea walipokuwa safarini jangwani kwa muda wa miaka 40.
Musa anasimulia matukio na sheria. Anatoa mwito wa utii na uaminifu kwa agano, upendo na ufuasi. Waisraeli wanaaswa kupokea mawaidha kwa unyenyekevu na shukrani. Msingi wa yote ni agizo la kuabudu Mungu wao peke yake na kumpenda kuliko vyote (5:6-7). Upendo, imani, unyenyekevu, uaminifu, uwajibikaji kwa Mungu na uadilifu vinavyodaiwa kutendwa na mwanadamu huasilika katika upendo wa Mungu (6:4-6). Aidha kitabu hiki kinaeleza juu ya siku za mwisho za maisha ya Musa na kifo chake pamoja na jinsi Yoshua alivyopokea uongozi.
Yaliyomo:
1. Utangulizi, Sura 1:1-5
2. Hotuba ya kwanza ya Musa uwandani Moabu, Sura 1:6–4:43
3. Hotuba ya pili ya Musa: Amri Kumi, Sheria mbalimbali, Maonyo na maagizo, Sura 4:44–28:68
4. Baraka na neema, Sura 29–30
5. Siku za mwisho wa maisha ya Musa, Sura 31–34

Iliyochaguliwa sasa

Kum UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha