Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kum 33:1-11

Kum 33:1-11 SUV

Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao. Hakika awapenda hayo makabila ya watu; Watakatifu wake wote wamo mkononi mwako; Nao waliketi miguuni pako; Watapokea kila mmoja katika maneno yako. Musa alituagiza torati, Ni urithi kwa mkutano wa Yakobo. Akawa mfalme katika Yeshuruni, Walipokutanika wakuu wa watu, Makabila yote ya Israeli pamoja. Reubeni na aishi, asife; Lakini watu wake na wawe wachache. Na baraka ya Yuda ni hii; akasema, Isikize, Ee BWANA, sauti ya Yuda, Umlete ndani kwa watu wake; Alijitetea kwa mikono yake; Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake. Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba. Aliyemtaja baba yake na mama yake, Mimi sikumwona; Wala nduguze hakuwakubali; Wala hakuwajua watoto wake mwenyewe; Maana wameliangalia neno lako, Wamelishika agano lako. Watamfundisha Yakobo hukumu zako, Na Israeli torati yako, Wataweka uvumba mbele zako, Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako. Ee BWANA, ubariki mali zake, Utakabali kazi ya mikono yake; Uwapige viuno vyao waondokao juu yake, Na wenye kumchukia, wasiinuke tena.

Soma Kum 33

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kum 33:1-11

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha