Kum 32:1-4
Kum 32:1-4 SUV
Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu. Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea. Maana nitalitangaza Jina la BWANA; Mpeni ukuu Mungu wetu. Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.