Kum 1:19-22
Kum 1:19-22 SUV
Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama BWANA, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea. Nami nikawaambia, Mmefika nchi ya vilima ya Waamori, anayotupa sisi BWANA, Mungu wetu. Tazama, BWANA, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike. Nanyi mkanikaribia kila mmoja wenu, mkasema, Na tupeleke watu mbele yetu, ili watupelelezee nchi na kutuletea habari za njia itupasayo kuipandia, na za miji tutakayoifikia.