Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mdo 27:33-38

Mdo 27:33-38 SUV

Na kulipokuwa kukipambauka Paulo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu cho chote. Basi nawasihi mle chakula, maana itakuwa kwa wokovu wenu; kwa maana hapana hata unywele wa kichwa cha mmoja wenu utakaopotea. Alipokwisha kusema hayo akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula. Ndipo wakachangamka wote, wakala chakula wenyewe. Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu mia mbili na sabini na sita. Walipokwisha kushiba wakaipunguza shehena ya merikebu, wakiitupa ngano baharini.

Soma Mdo 27

Video ya Mdo 27:33-38