Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 The UTANGULIZI

UTANGULIZI
Waumini wa Kanisa la Thesalonike hawakuelewa vema mafundisho ya Paulo kuhusu kurudi mara ya Pili kwa Kristo. Walidhani atarudi hivi karibuni. Wengine wakadhani siku ya Bwana imekwisha anza. Kwa hiyo waliacha kufanya kazi ya kujipatia riziki. Baada ya muda mfupi wa kuwatumia Waraka wa Kwanza, Paulo aliwatumia Waraka huu mwingine akiwa Korintho (Mdo 18:11).
Paulo aliuandika waraka huu kusahihisha wazo kwamba “Siku ya Bwana ilikuwa imekwisha fika” (2:2). Katika Waraka wa Kwanza kwa Wathesalonike ilisemwa kwamba kuja kwa Bwana kutakuwa ni jambo la ghafla bila kutazamia (1 The 5:1-11). Lakini katika Waraka wa Pili kwa Wathesalonike, ingawa hatuwezi kujua wakati wenyewe wa kuja kwake Bwana tunajua kwamba kuja kwake Bwana hakutakuwa mara. Jambo hili ni kwa sababu ya mapambano makubwa dhidi ya uovu sharti yafanyike kwanza; lakini hata hayo yatacheleweshwa kwa muda. Sehemu kiini katika Waraka huu ni 2:1-12 ambapo Paulo anasema juu ya ule uasi ambao lazima ufanyike kwanza (2:3-4,8), siri ya uasi (2:7) vitu ambavyo bila shaka walengwa wa Waraka huu walivijua vinatumika kuwaelezea Wathesalonike kwa nini Siku ya Bwana imekawia. Kwa ujumbe wa Waraka huu wa Pili kwa Wathesalonike, Paulo alilitayarisha kanisa la Thesalonike kuendelea na maisha ya hapa duniani: kuendelea kufanya kazi siku kwa siku kama yeye Paulo alivyofanya.

Iliyochaguliwa sasa

2 The UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha