Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Sam UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki kinaendeleza masimulizi ya Kitabu cha Kwanza cha Samweli kuhusu mfalme Daudi (angalia utangulizi wa Kitabu cha Kwanza cha Samweli). Daudi ni mtawala maarufu. Wakati wa utawala wake, Israeli limekuwa taifa moja na lenye nguvu. Daudi anaonekana kuwa mwenye imani thabiti na kumcha Mungu. Hata hivyo, udhaifu wake haukufichwa pia (11:1–12:12).
Masimulizi ya kitabu hiki yana mkazo kuwa uwezo na mamlaka vyenye kufaulu hutoka kwa Mungu. Kiongozi wa Israeli aliongoza kwa niaba ya Mungu na aliwajibika kwa Mungu. Hivyo badiliko la kutoka uongozi wa waamuzi kuwa uongozi wa kifalme lilipata kibali cha Mungu (1 Sam 8:7, 22).
Yaliyomo:
1. Utangulizi wa utawala wa Daudi, Sura 1–4
2. Ufalme wa Israeli ukiongozwa na Mfalme Daudi; Sura 5–10
3. Mfalme Daudi na Bathsheba, Sura 11–12
4. Balaa katika familia ya Daudi, Sura 13–20
5. Simulizi la nyongeza, Sura 21–24

Iliyochaguliwa sasa

2 Sam UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha