Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Sam 1

1
Daudi Awaomboleza Sauli na Yonathani
1 # 1 Sam 11:11; 30:17,26; 1 Fal 20:29,30 Ikawa baada ya kufa kwake Sauli, hapo Daudi aliporudi katika kuwaua Waamaleki, naye Daudi amekaa siku mbili katika Siklagi; 2#2 Sam 4:10; Mwa 37:29; 44:13; Hes 14:6; Yos 7:6; 1 Sam 4:12; Ayu 1:20; Mdo 14:14hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia. 3Daudi akamwambia, Umetoka wapi? Akamwambia, Nimeokoka katika kambi ya Israeli. 4#1 Sam 4:16Daudi akamwambia, Yalikwendaje? Tafadhali uniambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani, tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe, wamekufa. 5Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa? 6#1 Sam 31:1-6; 1 Nya 10:1-6Yule kijana aliyempa habari akasema, Nalikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi. 7Naye alipotazama nyuma, akaniona, akaniita. Nikajibu, Mimi hapa. 8Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki. 9Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu. 10#Amu 9:54Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nalijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikaitwaa ile taji iliyokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu. 11#Yos 7:6; 2 Sam 3:31; 13:31; 2 Nya 34:27; Ezr 9:3; Yoe 2:13Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye; 12wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa BWANA na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.
13Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Watoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki. 14#Hes 12:8; 1 Sam 24:6; Zab 105:15Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi#1:14,16 Au, mtiwa mafuta (taz. 1 Sam. 2:10). wa BWANA? 15#Amu 8:20; 1 Sam 22:17,18; 2 Sam 4:10; 1 Fal 2:25,34,46Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa. 16#1 Sam 26:9; 1 Fal 2:32; Lk 19:22Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi#1:14,16 Au, mtiwa mafuta (taz. 1 Sam. 2:10). wa BWANA.
17Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya; 18#Yos 10:13(kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema,
Wana wa Yuda na wafundishwe haya,
19Walio fahari yako, Ee Israeli
Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa;
Jinsi mashujaa walivyoanguka!
20 # Amu 16:23; 1 Sam 31:9; Mik 1:10; Kut 15:20; Amu 11:34; 1 Sam 18:6; 31:4 Msiyahubiri mambo haya katika Gathi,
Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni;
Wasije wakashangilia binti za Wafilisti,
Binti za wasiotahiriwa wakasimanga.
21 # Amu 5:23; Ayu 3:3,4; Yer 20:14; 1 Sam 10:1 Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu
Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo;
Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa,
Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.
22 # 1 Sam 18:4 Kutoka kwa damu yao waliouawa,
Kutoka kwa shahamu yao mashujaa,
Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma,
Wala upanga wa Sauli haukurudi bure.
23 # Amu 14:18 Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza
Maishani wala mautini hawakutengwa;
Walikuwa wepesi kuliko tai,
Walikuwa hodari kuliko simba.
24Enyi binti za Israeli, mlilieni
Huyo Sauli, ambaye aliwavika
Mavazi mekundu kwa anasa,
Akazipamba nguo zenu dhahabu.
25Jinsi mashujaa walivyoanguka
Katikati ya vita!
Ee Yonathani, wewe umeuawa
Juu ya mahali pako palipoinuka
26 # 1 Sam 18:1,3; 19:2; 20:17 Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu,
Ulikuwa ukinipendeza sana;
Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu,
Kupita upendo wa wanawake.
27Jinsi mashujaa walivyoanguka,
Na silaha za vita zilivyoangamia!

Iliyochaguliwa sasa

2 Sam 1: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha