Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Kor 3

3
Wahudumu wa Agano Jipya
1 # 2 Kor 5:12; Rum 16:1; Mdo 18:27 Je! Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa kuja kwenu, au kutoka kwenu? 2#1 Kor 9:2Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote; 3#Kut 24:12; 31:18; 34:1; Mit 3:3; 7:3; Rum 15:16; Yer 31:33; Eze 11:19; 36:26mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.
4Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 5#2 Kor 2:6Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. 6#Yer 31:31; 1 Kor 11:25; Rum 7:6; Yn 6:63Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. 7#Kut 34:29Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika; 8#Gal 3:2,5je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu? 9#Kum 27:26; Rum 1:17; 3:21Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi. 10#Kut 34:29Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana. 11Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.
12Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi; 13#Kut 34:33,35nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; 14#Rum 11:25ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; 15ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. 16#Kut 34:34; Rum 11:23,26Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. 17#Yn 7:39; 8:36; Kut 16:7; 24:17; Rum 8:2Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. 18Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

Iliyochaguliwa sasa

2 Kor 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha