Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Tim 2

2
Maagizo kuhusu Maombi
1 # Flp 4:6 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; 2kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. 3#1 Tim 1:1; 4:10Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; 4#Eze 18:23; 2 Pet 3:9ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. 5#Rum 3:29,30; Ebr 12:24Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 6#Gal 1:4; 2:20; Tit 2:14ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. 7#2 Tim 1:11; Gal 2:7,8Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.
8Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. 9#1 Pet 3:3-5Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10#1 Tim 5:10bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 11#Efe 5:22Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. 12#1 Kor 14:34; Mwa 3:16Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. 13#Mwa 1:27; 2:7,21-22; 1 Kor 11:8,9Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. 14#Mwa 3:1-6; 2 Kor 11:3Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. 15Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.

Iliyochaguliwa sasa

1 Tim 2: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha